Dodoma FM

Bushiri na mkewe kurudishwa A.Kusini

15 December 2020, 10:26 am

Mchungaji Shepherd Bushiri

Lilongwe,

Malawi.

Waziri wa usalama wa ndani wa Malawi , Richard Banda, amesaini nyaraka kwa ajili ya mchungaji tajiri na maarufu Shepherd Bushiri na mke wake, Mary kurudishwa nchini Afrika Kusini.

Hii inafuatia ombi la mahakama ya nchi jirani ya Afrika Kusini ambako Bushiri na mke wake Mary wanakabiliwa na mashitaka ya utakatishaji wa fedha na ufisadi.

Mahakama ya juu zaidi nchini Malawi iko tayari kuamua kuhusu kukamatwa kwa wawili hao baada ya kuachiliwa huru bila masharti na mahakama ya hakimu mkazi ambayo ilisema kuwa ilichukua uamuzi huo kwasababu hapakuwa na ombi rasmi la kumrejesha lililotolewa na Afrika Kusini.

Mchungaji Shepherd Bushiri

Mahakama itaamua kuhusu kesi hiyo tarehe 22 Disemba, kwa mujibu wa gazeti la Daily Times newspaper.

Bushiri na mke wake walitoroka kutoka Afrika Kusini mwezi uliopita, baada ya kukaidi sharti la kulipa dhamana ambayo ilikuwa inawazuia kuondoka nchini Afrika Kusini mpaka kesi yao itakapokamilika.

Mchungaji Shepherd Bushiri

Mchungaji huyo au Pastor Bushiri wakati huo alisema kuwa maisha yake yamo hatarini iwapo hataondoka nchini humo.