Dodoma FM

Abdulaziz Makame kuondoka Yanga

19 December 2020, 7:20 am

Dar es Salaama.

KIUNGO mkabaji wa Klabu ya Yanga Abdulaziz Makame yupo kwenye mpango wa kutua kwa mkopo ndani ya Klabu ya Polisi Tanzania. 

Taarifa zinadai kuwa mpaka sasa ni timu mbili zinahitaji kupata huduma yake ikiwa ni Polisi Tanzania  na Ihefu.

Sababu kubwa ya nyota huyo mzawa kuondoka ndani ya Yanga ni kukosa nafasi kikosi cha kwanza licha ya uwezo alionao.

Kocha Mkuu, Cedric Kaze amesema kuwa wachezaji ambao hawatumii bado wameshindwa kuonyesha uwezo.