Dodoma FM

Ole Gabriel:Elimu juu ya thamani ya mazao ya mifugo bado tatizo

2 March 2021, 1:25 pm

Na, Mariamu Matundu,

Dodoma.

Serikali imesema licha ya kuendelea kutoa elimu juu ya umuhimu wa minyororo mitano ya thamani ya mazao ya mifugo, bado Jamii imeendelea kupata changamato katika mnyororo wa mtaji watu pamoja na gharama.

Hayo yamesemwa na katibu mkuu ,Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof.Elisante Ole.Gabriel wakati akizungumza na Taswira ya Habari kuhusu hatua ambazo wameendelea kuzifanya, ili kuhakikisha jamii inapata elimu kuhusu Minyororo mitano ya thamani hiyo.

Prof.Ole Gabriel amesema kuwa bado jamii wanapata changamoto katika kukokotoa gharama, pamoja na kuajiri watu wenye Vigezo ambao watawezesha na Kuongeza thamani sekta ya Mifugo.

Kwa upande mwingine katibu mkuu Prof.Ole Gabriel ametaja mambo ambayo yalikuwa yanakwamisha sekta ya ngozi kuongezeka ni pamoja na kukosekana kwa ongezeko la thamani, hali ambayo imebadilika kutokana na mikakati ya Serikali.

Pamoja na hayo Prof.Ole Gabriel amesema kuwa mkakati wa wizara ni kuhakikisha sekta ya ngozi hakuna bidhaa itaachwa kutokana na ushauri wa wataalamu ambao wamekuwa bega kwa bega katika kuhakikisha bidhaa za Ngozi zinatumika bila kutupwa.