Dodoma FM

Baadhi ya sekta kuokoka na marufuku ya vifungashio vya plastiki.

17 March 2021, 2:09 pm

NA MARIAM MATUNDU

Afisa mazingira kutoka ofisi ya makamu wa rais Muungano na Mazingira Anamaria Gerome amesema kutokana na hilo baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu wametumia nafasi hiyo kutengeneza vifungashio vya plastiki  ambavyo vinatumika kama vibebeo.

Amesema mchakato wa kutafuta vifungashio mbadala tayari umeanza na mpaka sasa zaidi ya viwanda kumi na tano vimefika TBS na kupata maelekezo ya kuzalisha vifungashio vinavyofaa na tayari uzalishaji umeanza.

 Hayo yamefuatia muda wa siku tisini ulitolewa  Januari 8 hadi April 8 2021 kuhakikisha marufuku ya utengenezaji na usambazaji pamoja na matumizi ya vifungashio vya plastiki sokoni . H��`�

Imeelezwa kuwa marufuku  iliyo wekwa juu ya matumizi ya vifungashio vya plastiki haigusi vifungashio katika sekta ya afya, kilimo, mifugo, vyakula pamoja na vitunza taka.