Dodoma FM

ATCL yatengeneza hasara, ripoti ya CAG

8 April 2021, 12:00 pm

Na; Yussuph Hans.

Imeelezwa kuwa kwa Miaka Mitano mfululizo shirika la Ndege Tanzania ATCL imetengeza hasara ambapo kwa mwaka huu limesababisha hasara ya shilingi Bilioni sitini (60 ) na Milioni miambili arobaini na sita (246).

Hayo yamebainishwa  mbele ya waandishi wa habari jijini Dodoma.na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, (CAG) Bwana Charles Kichere wakati akisoma Ripoti ya Mwaka wa Fedha ulioishia June 30, 2020

Bwana Kichere amesema kuwa kupitia ukaguzi wa kiutendaji aliyoufanya katika Shirika la ndege Tanzania, amebaini hadi kufikia june, 30 2020 serikali ilikuwa imenunua ndege Nane kwa gharama ya Tsh trilion 1.28 katika juhudi za kufufua Shirika hilo ambapo kwa muda miaka mitano mfululizo kampuni hiyo imesababishia hasara Serikali.

Ameongeza kuwa katika Ripoti hiyo imebainisha kampuni tanzu zilizopata hasara ambazo ni kituo cha uwekezaji cha APC cha NBAA na PSSF, Kampuni ya uwekezaji na National Housing na PPF pamoja na kampuni TTCL.

Pamoja na hayo CAG Kichere amefanya ukaguzi katika halmashauri 64 katika ukusanyaji wa mapato na utekelezaji miradi mbalimbali kwa mwaka 2017/18, 2019/20 na kubaini mapungufu ya ukusanyaji wa mapato wa Tsh Bil 60 katika vyanzo mbalimbali.

Katika hatua nyingine Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG), Charles Kichere Kwa mwaka huu ametoa hati mbaya kwa Halmashauri ya Wilaya Shinyanga, Singida, Itigi na Igunga, Wilaya ya Sikonge, Urambo, Momba, Manispaa ya Tabora, Tume ya UNESCO na Hospitali ya Rufaa Morogoro.