Dodoma FM

Wananchi changamkieni fursa , Bomba la mafuta la hoima

12 April 2021, 12:48 pm

Na; Mariam Matundu.

Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani amewataka wananchi kujitokeza kuchangamkia fursa ambazo zitajitokeza Katika Hatua zote za Utekelezaji wa Ujenzi wa Mradi wa  kimkakati wa Bomba la Mafuta la hoima Mpaka Tanga ambao unaanza Mwezi huu .

Dk Kalemani ameyasema hayo leo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kiteto (CCM) Edward Ole Lekaita ambapo amesema  utekelezaji wa mradi huo unaanza Rasmi April Mwezi  huu na kukamilika 2023.

Amesema mradi huo ulitegemewa kuanza mwezi july utapita katika mikoa nane ,wilaya 24,vijijiji 127 na vitongoji 502  huku ukitarajia kutoa ajira 10000 katika hatua za awali .

Awali Naibu waziri wa Nishati Mh Stephen Byabato akijibu swali la Msingi la Mbunge Ole Lekaita amesema miongoni mwa wilaya ambazo bomba hilo litapita ni pamoja na kiteto hivyo wananchi watafaidika na ujenzi huo katika kufanya Biashara,Ajira pamoja na Fursa Nyingine za kichumi na kijamii.

Hata hivyo amesema Serikali kupitia Wizara ya Nishati na wadau  wengine wanaendelea kutoa Hamasa ili wananchi waendelee kunufaika na mradi wa bomba hilo katika shughuli za ujenzi na uendeshaji wa mradi.