Dodoma FM

Mlebe walia na ukosefu wa maji na umeme kijijini hapo

13 April 2021, 8:56 am

Na ;Victor Chigwada.

Wakazi wa kijiji cha Mlebe  Wilaya ya Chamwino wametoa shukrani  kwa wakala wa usimamizi wa barabarani vijijini TARURA  kwakupunguza adha ya ubovu wa barabara kijijini hapo.

Wakizungumza na Taswira ya habari Wananchi hao wamesema kuwa wanaishukuru TARULA kwa kurekebisha barabara inayotoka kijijini hapo hadi Mnase kwani ilikuwa haipitiki kutokana na kuharibiwa na mvua.

Mwenyekiti wa kijiji cha Mlebe Bw.Joseph Mpilimi amesema kwa sasa marekebisho hayo yamefikia asilimia 70 kwani bado barabara hiyo  haijafika mwisho kutokana na bajeti kuwa ndogo huku wakisubiri ahadi ya Mbunge aliyo waahidi baada ya Bunge la bajet kwisha.

Naye diwani wa Kata hiyo Bw.Eliasi Kaweya ameeleza kwamba kutokana na ufinyu wa bajeti waliamua kuangalia maeneo yaliyo athirika zaidi ikiwa ni pamoja na Mlebe ambako mkandarasi bado yupo saiti kuendelea na kazi.

Kata ya Mlebe licha ya kutatuliwa tatizo la miundombinu ya barabara iliyoharibiwa na mvua  lakini bado kata hiyo inakabiliwa na changamoto za ukosefu wa maji na umeme katika baadhi ya maeneo.