Dodoma FM

Tope lakwamisha shughuli za uvuvi Hombolo

15 April 2021, 11:42 am

Na; Victor chigwada

 

Wakazi wa Hombolo wanao jihusisha na shughuli ya uvuvi wamelalamikia bwawa hilo kujaa tope  na kupungua kina hali inayo sababisha vifo kwa wavuvi wanao kwama kwenye tope hilo.

Wakizungumza na taswira ya habari wavuvi hao kutoka Hombolo A wamesema kutokana na bwawa hilo kujaa tope na kupungua kina shughuli ya uvuvi imepungua kwani mara nyingi wavuvi  hao wanapo  kuwa kwenye shughuli ya uvuvi  baadhi yao hukwama  kwenye tope na kupoteza maisha.

Nae mwenyekiti wa mataa wa Hombolo A Bw.Gerad Mtangwa amesema bwawa hilo  kwasasa limepungua kina kutoka na kujaa tope hivyo wanaomba msaada wa kupatiwa wataalamu wa kuchimba mabwawa ili waweze kuondoa tope hilo.

Taswira ya habari ilizungumza na  Afisa Mtendaji wa mtaa huo wa Hombolo A bw.Wilisoni Nyonge yeye anasema bwawa la Hombolo limechimbwa kipindi kirefu sana hali inayo pelekea bwawa hilo kwasasa kujaa tope ambalo limekuwa chanzo cha vifo vya wavuvi wengi wanao kwama kwenye tope hilo.

Bwawa la hombolo  lipo umbali wa kilomita 45 kutoka katikati ya jiji la Dodoma , ni bwawa la muda mrefu ambalo limekuwa likiwasaidia wakazi wa eneo hilo kufanya shughuli mbalimbali kupitia maji yanayo patikana kwenye bwawa hilo ikwemo kilimo  pamoja na uvuvi.