Dodoma FM

Changamoto ya Maji safi na salama kijiji cha Banyibanyi bado yakosa ufumbuzi

19 April 2021, 1:23 pm

Na; Selemani Kodima

Licha ya Jitihada mbalimbali kuendelea kufanyika ,Bado kijiji cha Banyi banyi wilayani Kongwa kimeendelea kukabiliwa na Changamoto ya ukosefu wa maji safi na salama.

Hili limeendelea kujiri baada ya Kupitia zaidi ya Mwezi mmoja tangu Uongozi wa kijiji hicho kuanisha mkakati wa kutafuta Ufumbuzi wa upatikanaji wa maji safi na salama kwa kuanza kurekebisha Kisima cha maji .

Mwenyekiti wa kijiji cha Banyi banyi Bw Silas Magoa kujua hali ipoje licha ya taarifa ya mwisho kuainisha wapo katika mpango wa kuunganisha Umeme katika kisima cha maji .

sauti ya Mwenyekiti wa kijiji cha Banyi banyi Bw Silas Magoa

Amesema jambo ambalo limechelewa kijiji hicho kuwa na maamuzi kupitia mkutano wa kijiji ni kutokana na kukosekana kwa mtendaji wa kijiji hali ambayo wameshindwa kuwashirikisha wananchi juu ya Changamoto hiyo.

Suala la Changamoto ya maji katika kijiji cha Banyi Banyi sio tatizo la leo tu,bali ni suala ambalo limepitia mengi Katika historia ya wakazi wa eneo hilo .