Dodoma FM

Rais Samia awashukia wabunge kuhusu mijadala isio na tija kwa taifa

19 April 2021, 5:41 am

Na ; Mariam kasawa     

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.  Samia Suluhu Hassan amesikitishwa na mijadala inayoendelea bungeni ya kumlinganisha na mtangulizi wake,   hayati John Magufuli.

Akizungumza jana Jumapili Aprili 18, 2021 katika kongamano la viongozi wa dini,   Samia amesema yeye na Magufuli ni kitu kimoja na anaendeleza kazi iliyofanywa na mtangukizi wake huyo aliyefariki dunia Machi 17, 2021 kwa ugonjwa wa moyo.

 Amesea “Inasikitisha sana kuona watu wanapiga ngoma mitandaoni na inachezwa bungeni  tena inachezwa kwa umaridadi, mmejikita kulinganisha watu badala ya ajenda, mnalinganisha Magufuli na Samia”.

Aidha amesema  yeye na hayati Magufuli  ni kitu kimoja,  hivyo amewataka  wabungeni kujikita kwenye bajeti za wizara mbalimbali mengine yatajadiliwa badae.