Dodoma FM

Ushirikiano watakiwa kukomesha wizi wa maji Dodoma

19 April 2021, 12:19 pm

Na; Benard Filbert.

Mafundi wa DUWASA wakifanya matengenezo ya bomba katika kituo cha kusukumia Maji cha Mailimbili

Wenyeviti wa mitaa katika jiji la Dodoma wametakiwa kutoa ushirikiano kwa mamlaka ya maji DUWASA ikiwepo kutoa taarifa za watu wanaojiunganishia maji kinyume na sheria.

Hayo yanajiri kufuatia agizo la mkuu wa Mkoa Dkt.Binilith Mahenge alilolitoa hivi karibuni akiwataka wenyeviti wa mitaa kushirikiana na DUWASA kuzuia upotevu wa maji hali inayochangia hasara kwa mamlaka hiyo.

Bw.Matwiga Kiatya amesema maagizo hayo yameamsha ari ya kuanza ufuatiliaji katika Mtaa wake kwa kushirikina na viongozi wenzake.

Sauti ya mwenyekiti wa wenyeviti jiji la Dodoma

Kadhalika amewataka wananchi kutumia maji kwa utaratibu maalumu na kuepuka kuharibu miundombinu ya maji ili kuleta ufanisi kwa mamlaka hiyo pasipo vikwazo.

Sauti ya mwenyekiti wa wenyeviti jiji la Dodoma

Hivi karibuni mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk.Binilith Mahenge kwa kushirikiana na mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Dodoma DUWASA, walikutana na wenyeviti wa mitaa mbalimbali na kuwataka kushirikiana na mamlaka hiyo kufichua wananchi wanaojiunganishia maji kinyume na taratibu.