Dodoma FM

Wakulima washauriwa kutumia njia bora za kuhifadhi mazao

21 April 2021, 7:52 am

Na ;Thadei Tesha.

Wakulima wameshauriwa kutumia njia bora za uhifadhi wa mazao ili kuhakikisha mazao yao yanadumu kwa muda mrefu bila ya kuharibika.

Akizungumza na taswira ya habari afisa kilimo wa jiji la Dodoma Bi.Gloria Woisso amebainisha njia bora za uhifadhi ni pamoja na kutumia mifuko maalum,vihenge na madawa kwa kufuata maelekezo ili kuepusha madhara ya kiafya.

Kwa upande wake mkuu wa idara ya kilimo katika Halmashauri ya jiji la Dodoma Bi.Yustina Munishi amesema wakulima wanapaswa kupata elimu sahihi juu ya njia bora ya uhifadhi kwa njia ya madawa na kuwataka kuacha mara moja kuacha kutumia sumu ambazo hazijathibitishwa.

Nao baadhi ya wakulima jijini hapa wameelezea njia wanazotumia kuhifadhi mazao yao ambapo wamebainisha kuwa mara nyingi wamekuwa wakitumia mifuko na dawa maalum.

Wakulima wengi wamekuwa wakilalamikia mazao yao kuharibika mara baada ya kuvuna kutokana na kutumia njia zisizo sahihi za kuhifadhia.