Dodoma FM

Rais Samia Suluhu afanya uteuzi mwingine

23 April 2021, 2:58 pm

Na; Ikulu Mawasiliano

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Hedwiga Swai kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania.

Dkt. Swai anashika wadhifa huo kwa kipindi cha pili baada ya kipindi cha kwanza kumalizika.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Samia amemteua Bi. Sophia Elias Kaduma kuwa Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS).

Uteuzi wa viongozi hao umeanza leo tarehe 23 Aprili, 2021.