Dodoma FM

Changamoto ya Madawati shule ya sekondary Wotta yatatuliwa

27 April 2021, 10:00 am

Na; Seleman Kodima

Wakazi wa kata ya Wotta  wilayani Mpwapwa wameishukuru  Dodoma fm redio kwa Juhudi ya  kubwa walizofanikisha kuripoti tatizo la uhaba wa madawati ktika shule ya sekondari  na hatimaye Changamoto hiyo kufanyiwa kazi .

Hayo yamejiri baada ya kituo hiki kuripoti changamoto ya uhaba wa madawati katika shule ya sekondari Wotta  inavyoathiri ukaaji na umakini wa watoto wawapo darasani.

Wakizungumza na Taswira ya habari baadhi ya wakazi  wa eneo hilo wamesema zoezi la kutatua changamoto ya madawati  shuleni hapo limekwisha anza  ambapo mafundi wana endelea na zoezi la utengenezaji wa Viti na meza .

Nae Diwani wa kata hiyo Bw. Mugabe Athumani amesema zoezi la utengenezaji wa Viti na meza linaendelea huku  wananchi wa Vijiji vyote ndani ya kata yake wakishiriki kikamilifu katika hatua zote za utengenezaji madawati hayo .

Aidha amewataka wananchi kuendelea kuchangia michango mbalimbali pale inapohitajika kuhusu masuala mbalimbali ya kimaendeleo ndani ya kata yao.

Hivi karibu Taswira ya habari iliripoti kuhusu uhaba wa madawati katika shule ya wotta hali ambayo imefanyiwa kazi na Uongozi wa kata hiyo kwa kushirikiana na wananchi.