Dodoma FM

Tanzania yaadhimisha miaka 57 ya muungano

27 April 2021, 6:10 am

Na,Mariam Matundu.

Ikiwa Tanzania imeadhimisha miaka 57 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar ,imeelezwa kuwa changamoto 15 kati ya 25 za muungano zimetatuliwa .

Hayo yameelezwa na Makamu wa Rais Dr. Philip Mpango wakati akifungua kongamano la maadhimisho ya miaka 57 ya muungno wa Tanzania na kuongeza kuwa jitihada zinaendelea ili kumaliza changamoto zilizosalia.

Makamu wa rais  amesema kwa kushirikiana na viongozi wa serikali za pande mbili katika kuulinda na kuuenzi muungano na kwamba hata wafumbia macho wale wote watakao jaribu kuuvunja muungano.

Aidha amesema miaka 57 ya muungano imesaidia kuimarika kwa umoja ,usalama ,kukua na kuimarika kwa shughuli za kibashara na kwamba serikali zote mbili Tanzania na Zanzibar zimeweka suala la muungano kuwa ni kipaumbele.

Nae Jawadu Mohamed ambae ni mchambuzi wa masuala ya kisiasa amesema teuzi mbalimbali za viongozi zinazofanywa na mh Rais Samia Suluhu Hassani kwa kuzingatia uwepo wa pande zote mbili za muungano zinaendelea kuimarisha muungano wa Tanzania.

Kongamano la muungano limefanyika kwa lengo la kukuza ufahamu na uelewa kuhusu muungano huku sherehe za muungano zikiwa zimebebwa na kauli mbiu isemeyo MUUNGANO WETU NI MSINGI  IMARA WA MAPINDUZI KIUCHUMI TUDUMISHE MSHIKAMANO WETU.