Dodoma FM

Serikali kutunga sheria uvunaji wa viungo

29 April 2021, 6:35 am

Na;Yussuph Hans.

Naibu Waziri wa Afya, Godwin Mollel, amesema kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya upandikizaji wa viungo Nchini, Serikali imeandaa Muswada wa kutunga Sheria itakayoongoza taratibu za uvunaji, utunzaji na upandikizaji wa viungo

Ameeleza hayo bungeni jijini Dodoma wakati akimjibu Mbunge wa Viti Maalum, Rose Tweve, aliyehoji kuhusu mkakati wa Serikali kuanzisha utaratibu maalum wa kuvuna viungo vya Binadamu kama Figo na Moyo kwa ajili ya wenye uhitaji

Naibu Waziri amesema kuwa, Kwa kuwa huduma zimeanza kutolewa, kwa sasa Nchi inatumia miongozo ya kimataifa kusimamia uvunaji na upandikizaji wa viungo

Kwa upande mwengine Mbunge wa Viwawa, Japhet Hasunga amesema kwa mujibu wa Sheria, Ushirika ni kwa Wanaushirika wenyewe lakini hali ilivyo sasa, Ushirika umekuwa ukiwalazimisha watu wasio Wanachama kuuza mazao yao kupitia kwenye Vyama vya Ushirika

Akiwa Bungeni Dodoma, Hasunga ambaye amewahi kuwa Waziri wa Kilimo ameuliza kuwa, Serikali haioni ulazima wa kuruhusu Kampuni Binafsi na Wafanyabiashara kununua moja kwa moja kwa Wakulima bila kupitia Ushirika.

Akimjibu, Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema, serikali ina imani mfumo wa Ushirika ndio njia sahihi ambayo itamsaidia Mkulima mdogo kupata Haki yake kwa urahisi zaidi.