Dodoma FM

Vijana nchini washauriwa kujihusisha na shughuli za kilimo

7 May 2021, 12:42 pm

Na; FREDY CHETI . 

                                     

  vijana nchini wameshauriwa kujihusisha na shughuli za kilimo ili waweze kujiajiri na kuendesha maisha yao.

Wito huo umetolewa na Bi. Lucy Madala mtaalamu wa kilimo kutoka chuo kikuu cha kilimo (SUA) wakati akizungumza na  taswira ya habari wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya kitaifa ya Sayansi na Teknolojia (MAKISATU)  yaliyoandaliwa na wizara ya Elimu jijini Dodoma ambapo amesema kuwa zipo teknolojia nyingi za kisasa ambazo vijana wanaweza kujifunza na kuzitumia kuzalisha bidhaa mbalimbali  kupitia kilimo zitakazoweza kuwasaidia kuwainua kiuchumi

Aidha Mtaalamu huyo amewataka wakulima nchini kutumia kilimo cha kisasa zaidi ambacho kinaweza kuwapatia mazao mengi tofauti na kilimo cha kizamani na kuacha kuhofia gharama kwani kuna njia nyingine za kisasa ambazo hazina gharama yoyote.

Taswira ya habari imezungumza na baadhi ya vijana jijini hapa juu ya suala hilo ambapo wamesema kuwa vijana wengi hasa waliopo mijini wanakimbia vijijini na kwenda mjini  kwa lengo la  kutafuta maisha jambo ambalo husabisha wengi kubaki bila shughuli yoyote hivyo  ni vyema elimu zaidi ikatolewa juu ya utajiri uliopo katika kilimo ili wajikite zaidi katika shughuli hizo.

Licha ya kilimo kuwa uti mgongo kwa Taifa kwa kuchangia uchumi mkubwa  bado kundi kubwa la vijana bado linaona kilimo ni utumwa na sio kama ajira zingine huku kundi hilo dogo limekuwa likiendelea  na kilimo cha mazoea hali inayofanya wengi wao kushindwa kupata mafanikio ya haraka hivyo ni vyema vijana wakachukua hatua zaidi  ili kufikia mafanikio yao.