Dodoma FM

Kigwe waililia serikali maji safi na salama

25 May 2021, 11:57 am

Na; Victor Chigwada

Wananchi wa Kijiji cha Mapinduzi Kata ya Kigwe Wilaya ya Bahi wameiomba Serikali na taasisi binafsi kuwatatulia changamoto ya uhaba wa maji safi na salama.

Wakizungumza na taswira ya habari baadhi ya wananchi hao wamesema kwa muda mrefu sasa wamekosa huduma hiyo ambapo  miundombinu ya maji iliyopo ni chakavu kwa kuwa ni ya muda mrefu.

Mtendaji wa Kijiji hicho Bw.Adeunisi Audivansi pamoja na kukiri  kuwepo changamoto hiyo, amesema wameanzisha mradi mdogo wa maji wa Kata ili kuwatatulia wananchi adha hiyo.

Naye Diwani wa Kata ya Kigwe Bw.Joseph Mkwawa amesema tayari amefikisha suala hilo kwenye vikao vya Halmashauri, ambayo imewasidia kupata mfadhili wa kukamilisha mradi wa kitongoji cha madukani  huku wakisubiri bajeti kutoka Serikalini kukamilisha mradi mkubwa.

Serikali kupitia Wakala wa maji na usafi wa mazingira Vijijini RUWASA imeendelea kufanya jitihada za kusogeza huduma ya maji karibu na wananchi ili kuwapunguzia usumbufu wa kutembea umbali mrefu.