Dodoma FM

Wakazi Farkwa walazimika kupanda juu ya miti kupata mawasiliano ya simu

26 May 2021, 12:59 pm

Na; Victor Chigwada

Wananchi wa Kata ya Farkwa Wilaya ya Chemba wanakabiliwa na changamoto ya uhafifu wa mawasiliano ya simu za mkononi kutokana na uhaba wa minara

Baadhi ya wananchi hao wakizungumza na taswira ya habari wamesema kuwa wanalazika kutafuta sehemu za miinuko au kukaa kwenye miti ili kuwasiliana hivyo wameiomba Serikali na wadau wa mawasiliano kuwasidia kujenga minara

Mwenyekiti wa kijiji cha Bubutole Bw.Hosea Ndalami amekiri eneo lake kukabiliwa na changamoto ya mawasiliano licha ya kuwepo kwa mnara mmoja katika kitongoji chake ambao haukizi mahitaji ya watumiaji

Naye Diwani wa Kata hiyo Bw.Stephani Patrick amesema kutokana na changamoto hiyo kwa kata nzima ni vijiji viwili ambavyo unaweza kuwapata kwa njia ya mawasiliano ya simu za mkono

Aidha ameongeza kuwa hali hiyo inawasababishia kupata ugumu katika shughuli za kiutendaji ikiwa ni pamoja yanapotolewa maagizo na taarifa mbalimbali kutoka wilayani inakuwa ni vigumu kuwapa taarifa baadhi ya vijiji

Kutokana na changamoto ya mawasiliano katika maeneo ya vijijini Serikali imeendelea na utoaji ruzuku na zabuni za kuwawezesha ujenzi wa miundombinu ya mawasiliano katika Kata ambazo hazijafikiwa