Dodoma FM

Elimu ya ufundi ni kichocheo bora cha maendeleo endelevu Nchini.

27 May 2021, 2:04 pm

Na;Mindi Joseph.

Serikali imesema maendeleo ya viwanda na usatawi wa jamii hayawezi kuleta tija pasipo kuwa na usimamizi bora kwenye elimu ya ufundi kama kichocheo endelevu cha ukuaji wa uchumi nchini Tanzania.

Akizungumza katika Ufunguzi kongamano la wadau wa elimu ufundi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama amesema Tanzania imepiga hatua katika ukuaji wa uchumi kwa kipindi cha miaka 5 na ukuaji huo wa uchumi umeshabihiana na dhana ya ufundi.
Waziri Mhagama ameongeza kuwa ulimwengeni kote elimu na mafunzo ya ufundii ndio njia pekee inayotoa mchango mkubwa katika ujenzi wa uchumi.

Kwa upande wake katibu mtendaji wa Nacte Dkt.Adolf Rutayuga amesema kupitia kongamano hilo itasaidia kubaini namna ya kutoa elimu ya ufundi itakayojibu matatizo ya kiuchumi katika jamii na kukuza ushirikiano baina ya vyuo vya elimu ya ufundi na mafunzo na waajiri.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi NACTE, Prof. John Kandoro amesema hali ya uwekezaji wa sekta binafsi katika vyuo vya sanyansi na teknolojia shirikishi ni mdogo sana ikilinganishwa na vyuo vingine na kuiomba serikali kuelekeza nguvu katika uwekezaji wa vyuo vya sanyansi na teknolojia shirikishi ili kuhakikisha uchumi wa kati na wa juu unafikiwa.

Maonesho ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi yatafunguliwa rasimi kesho na Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh Kasim Majaliwa katika uwanja wa jamhuri jijini Dodoma lengo la maonesho hayo ni kuchochea ukuaji wa ushirikiano kati ya wadau na vyuo vya mafunzo katika utoaji wa elimu bora inayokusudiwa na jamii.