Dodoma FM

Kata ya Nzuguni washangilia Neema ya umeme kupitia mradi wa REA

27 May 2021, 1:08 pm

Na ;Victor Chigwada

Wakazi wa mtaa wa Nzuguni A Jijini Dodoma wamepata matumaini ya kupata huduma ya nishati ya umeme baada ya zoezi la usambazaji nguzo kupitia mradi wa REA kuanza katika eneo hilo.

Baadhi ya wakazi wa eneo hilo wakizungumza na taswira ya habari wamesema usambazaji wa nguzo za umeme unaendelea licha ya kuwa na changamoto ya upatikanaji wa fomu ili wananchi wanaohitaji kupata huduma hiyo waweze kujaza.

Nae Mwenyekiti wa mtaa wa Nzuguni A Bw. Onaely Mbatian amesema tayari wakandalasi wapo eneo la kazi hivyo amewakumbusha wananchi kwenda kuchukua fomu katika ofisi za TANESCO zitakazo wawezesha kupatiwa huduma ya umeme.

Bw.Aloyce Luhega ni diwani wa kata ya Nzuguni yeye anasema lengo lao ni kusambaza umeme katika mitaa yote hivyo ametoa wito kwa wakazi wa eneo hilo kuwa bei ya umeme kwa walio karibu na nguzo za zamani na mpya ni moja .

Umeme unaotolewa na wakala wa umeme vijijini REA haumtozi mwananchi gharama ya fomu za maombi ya kuunganishiwa umeme kwani gharama hizo zimebebwa na Serikali.