Dodoma FM

Wafanyabishara waiomba serikali kurahisisha usafirishaji wa mizigo

1 June 2021, 6:09 am

Na; Benjamin Suluwano.

Wafanyabiashara wa soko la sabasaba wameiomba serikali kutafuta njia mbadala ya kurahisisha usafirishaji wa mizigo kutoka soko la Job Ndugai kwenda sokoni .

Wakizungumza na Dodoma fm baadhi ya wafanyabiashara wamesema wanaomba wapunguzie ushuru na serikali iongeze tani za ujazo wa mzigo hadi kufikia tani tatu ili kurahisisha usafirishaji wa mizigo yao.

Nae kaimu mwenyekiti wa soko Bw Kombo amethibitisha kuwepo kwa changamoto ya usafirishaji wa mizigo ya wafanyabiashara kutoka Ndugai kuja sokoni ,hivyo ameiomba serikali kama ni malipo yote yafanyike sokoni Sabasaba ili kupunguza gharama za usafiri .