Dodoma FM

Upanuzi wa bwawa Bubutole wapelekea wananchi kukosa huduma za kijamii

21 June 2021, 9:50 am

Na; Victor Chigwada.

Wakazi wa kijiji cha Bubutole wilayani Chemba wamelalamika kukosa baadhi ya huduma za kijamii kutokana na utanuzi wa bwawa unao endelea kijijini hapo.

Wakizungumza na taswira ya habari wananchi hao wamesema tangu kutangazwa kwa utanuzi wa bwawa hilo wamekuwa wakikosa huduma ya umeme pamoja na maji kwani waliamriwa kuhama katika eneo hilo baada ya malipo kukamilika.

Nae mwenyekiti wa kijiji hicho Bw.Hosea Ndalami amekiri kuwa wakazi wa eneo hilo hawapatiwi huduma ya umeme pamoja na maji kwa wanatakiwa kuhama katika eneo hilo lakini bado hawajakamilishiwa malipo yao.

Taswira ya habari ilizungumza na diwani wa Kata ya Farkwa Bw.Stephano Patrick yeye amewataka wananchi ambao wamekwisha kamilishiwa malipo yao waanze kupisha eneo hilo kwaajili ya upanuzi wa bwawa na ambao hawajalipwa waendelee kuwa na subira watapewa malipo yao.

Ujenzi wa bwawa la farkwa ni moja ya mikakati ya kutatua tatizo la maji katika Mkoa wa Dodoma kwani bwawa hilo litapitisha maji kutoka ziwa Victoria.