Dodoma FM

Jamii yatakiwa kujifunza ili kuepusha matukio yanayo tokea

27 July 2021, 1:13 pm

Na; Shani Nicolous.

Kufuatia kwa matukio mbalimbali ya moto katika jamii hususani wanawake kuchoma nyumba za wananume kwa wivu wa mapenzi jamii imetakiwa kufunguka na kujifunza namna ya kuepusha matukio hayo.

Akizungumza na Dodoma fm Mwanasaikolojia kutoka shirika la kisedet Bw. Mtahu Mtahu amesema kuwa wengi hufanya hayo matukio mabalimbali kwa kulimbikiza kisasi vinavyotokana na wivu wa kimapenzi.

Ameongeza kuwa visasi na hasira si suruhisho la kuyajenga mapenzi hayo vinginevyo ni sababu ya kutafuta kesi na kurudishana nyuma kimaendeleo kwa kupoteza nyumba na vitu vya thamani.
Amesema kuwa uaminifu katika mahusiano ndiyo unaotakiwa ili kuepusha na kukomesha matukio yasiyokuwa yalazima ambayo ni fedheha katika jamii .

Kwa upande wao baadhi ya wananchi jijini hapa wamesema kuwa tabia hii baadhi ya wanawake wamechukulia ni mtindo kutokana na kufuatana kwa matukio yakufanana wamesema serikali ichukue hatua kali kwa yeyote atayebainika akifanya matukio hayo.

Wivu wa kimapenzi umekuwa ni sababu ya matukio mbalimbali ya kiharifu yanayoendelea kutokea katika jamii hususani matukio vya vifo kwa kuchomana moto na hata kuunguza mali kwani ndani ya mwezi huu yameripotiwa matukio mfululizo yanayofanana.