About us

Hayo yamezungumzwa na baadhi ya wananchi wa kijiji hicho ambapo wamesema kuwa wanatumia maji ya taasisi za kidini kuliko maji yanayotoka kwenye mradi wao kwasababu wasizozifahamu.

“upatikanaji wa maji katika mradi wetu sio mzuri tunapata maji kupitia taasisi za kidini kuliko mradi wetu wa kijiji hii ni changamoto tunayoipata na wakati mwengine tunajiuliza kama sio hizi taasisi tungekuwa wapi sisi wananchi”

Aidha mwenyekiti wa kijiji hicho bwana MNYIMBONI HAMISI amesema kuwa mradi huo ulivunjwa na muheshimiwa AWESO kutokana na kutosomwa mapato na matumizi yanayoingia katika mradi huo.

“kamati ya maji katika kijiji hichi haifanyi vizuri na ndio mana muheshimiwa mbunge ambaye pia ni naibu waziri wa maji JUMAA AWESO alivunja kamati ya maji na kuikabidhi mamalaka ya maji mjini pangani kutokana na kutosomwa kwa mapato na matumizi”

Akijibia changamoto hiyo ya upatikanaji wa maji katika kijiji cha Madanga muhandisi wa maji wilaya bwana NOVAS WILSON amesema taarifa ya changamoto hiyo haijamfikia na kuwataka wannachi hao kutoa taarifa mapema kunapotokea changamoto ili tatizo liweze kushuhulikiwa.

“pindi kunapotokea changamoto yoyote katika mradi ni lazima taarifa zitufikie na endapo kamati wanataka kuboresha mradi wa maji pia taarifa zifike ofisini ili sisi tujuwe ni kwa namna gani tunatatua changamoto hiyo ili wananchi waweze kupata huduma ya maji”

Kamati ya maji katika kijiji cha madanga jaira ilivunjwa na muheshimiwa mbunge baada ya utendaji mbovu na kusuasua kwa mradi huo na kukabidhiwa mamlaka ya maji pangani mjini.

  1. Jamii wilayani Pangani mkoani Tanga imetakiwa kushiriki kikamilifu katika kupiga vita vitendo vya rushwa nchini ili kusaidia taifa kupiga hatua katika masuala ya kimaendeleo.
  2. Hayo yamezungumzwa na Kiongozi wa Mbio za mwenge kitaifa mwaka huu 2019 ndugu MZEE MKONGEA ALLY wakati wa akizindua klabu ya kupinga rushwa inayoundwa na baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya masista wa ivumoni ambapo amesema mapambano ya rushwa ni ya jamii yote.

MAAJABU YA DJ WAR PANGANI FM

Sehemu ya Matukio katika kuwasili kwa Mwenge wa Uhuru Wilayani Pangani Mkoani Tanga.

  • Mwenge wa uhuru unatarajiwa kufika wilayani pangani mkoani tanga na kukimbizwa katika viunga vyake Tarehe 6 mwezi huu wa 7 ukienda sambamba na kufungua miradi mbali mbali ya maendeleo wailayani humo.
  • Hayo yamezungumzwa na Bwana Isaya Mbeje ambaye ni mkurugenzi wa halmashauri wa wilaya ya Pangani wakati akifanya mahojiano maalaum na Pangani Fm kuhusiana na ujio wa mwenge wa uhuru,Ambapo amesema kuwa Mwenge wa uhuru unatarajiwa kufika wilayani pangani Tarehe 6 mwezi huu uk.