Huheso FM

TAKUKURU yasimamisha ujenzi jengo la X-RAY halmashauri ya Msalala

April 21, 2021, 5:02 pm

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) wilayani Kahama mkoani Shinyanga imezuia kuendelea ujenzi wa jengo la X-RAY kituo cha Afya Bugarama katika halmashauri ya Msalala kutokana na matofali yanayotumika kuwa chini ya kiwango.

Mkuu wa TAKUKURU wilayani Kahama, Abdallah Urari amesema katika ufuatiliaji wa taasisi hiyo ikishirikiana na mhandisi wa ujenzi halmashauri ya Msalala ilibaini matofali zaidi ya Elfu tatu yasiyo na ubora yaliyopelekwa na mzabuni Block Traders katika ujenzi huo.

SAUTI YA MKUU WA TAKUKURU WILAYA YA KAHAMA

Nae mkurugenzi wa halmashauri ya Msalala, Simon Berege baada ya kupokea taarifa hiyo amemuagiza mhandisi wa ujenzi wa halmashauri hiyo kumtaka mzabuni husika kuondoa matofali hayo mara moja na taratibu zingine za manunuzi zifanyike kumpata mzabuni mpya.

Hata hivyo mradi wa ujenzi huo katika kituo hicho cha Bugarama linatarajiwa kutumia jumla ya shilingi milioni 53 hadi kukamilika ikiwemo gharama za ununuzi wa vifaa pamoja na gharama za ufundi.

MWISHO