Huheso FM

Wafanyabiashara wamlalamikia Mkurugenzi Manispaa ya Kahama

May 18, 2021, 6:28 pm

Picha ya wafanyabiashara wa soko la CDT manispaa ya Kahama

Wafanyabiashara wanaozunguka eneo la kituo cha mabasi katika Kata ya Majengo iliyopo Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga wamemlalamikia Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kuyarudisha mabasi ya abiria katika kituo cha mabasi  iliyokuwa ikikarabatiwa ya CDT.

Wakizungumza na waandishi wa habari wafanyabiashara hao wamesema mara baada ya mabasi ya abiria kuondoka katika standi hiyo hali ya kibiashara imekua ngumu hali iliyopelekea baadhi yao kufunga biashara.

Sauti za wafanayabiashara wa eneo la kituo cha mabasi

Kwa upande wake diwani wa Kata ya Majengo, Bernad Mahongo amesema hajashirikishwa kikamilifu kwenye mchakato wa kuyarudisha mabasi hayo eneo lake la awali.

Sauti ya diwani kata ya Majengo

Akizungumzia suala hilo mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama Anderson Msumba amesema kituo cha mabasi cha CDT ni kituo halali cha mabasi na wamachinga.

Sauti ya Mkurugenzi wa manispaa ya Kahama

Hata hivyo Mwaka jana mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama aliamuru kuhamishwa kwa mabasi ili kupisha ukarabati eneo la stendi ya CDT na mara baada ya kukamilika ukarabati mkurugenzi huyo ameelekeza baadhi ya mabasi hayo kurudi katika eneo lake la awali.