Jamii FM

Ajiua kwa wivu wa Mapenzi

18 January 2021, 11:43 am

Mtu mmoja aliejulikana kwa jina la Chikwisu mkazi wa Majengo Newala mjini amefariki dunia baada ya kujimwagia mafuta ya petrol mwilini na kujichoma huku kisa kikitajwa kuwa ni ugomvi wa kimapenzi na mke wake

Awali akizungumza na Newala FM mtoto wa marehemu Msafiri Hashimu amesema chanzo cha Baba yake kufanya hivyo ni baada ya marehemu kumfumania mke wake takribani wiki moja iliyopita ambapo baada ya tukio hilo marehemu hakuwa sawa hali iliyopelekea kujiua

Kabla ya umauti wake mganga mkuu wa halmashauri ya mji Newala daktari Joseph Fwoma amethibitisha kumpokea Chikwisu na wakati anapatiwa matibabu alifariki dunia, Dkt Joseph Fwoma amesema marehemu aliungua kwa kiasi kikubwa kuanzia kichwani mpaka maeneo ya tumboni.