Jamii FM

Wawezeshaji TASAF wasisitizwa kutumia weledi uibuaji miradi

24 February 2021, 04:45 am

Timu ya wataalamu wa sekta mbalimbali halmashauri ya wilaya mtwara imeendelea na mafunzo ya siku sita yatakayowawezesha kusaidia uibuaji wa miradi ya kipindi cha ari kwa walengwa wa kaya maskini kupitia mradi wa TASAF kunusuru kaya maskini awamu ya tatu sehemu ya pili unaoendelea katika jumla ya Vijiji 57.

wataalamu wa sekta mbalimbali halmashauri ya wilaya Mtwara wakiwa katika mafunzo ya siku sita ua uibuaji miradi kupitia TASAF

Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo na ubunifu wawezeshaji wa mpango wa kunusuru kaya maskini kutoka sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi, ujenzi, mazingira, afya, ardhi ambapo mara baada ya mafunzo watajikita vijijini kwaajili ya kuwasaidia walengwa kuibua miradi itakayowawezesha kujiongezea kipato kwa kipindi chote cha hali ngumu.

Akiongea na waandishi wa habari wakati wa mafunzo hayo, mmoja wa wawezeshaji ngazi ya halmashauri Bwana Hassan Dadi ametanabaisha kuwa, mara nyingi elimu wanayopata inasaidia katika kuibua miradi yenye tija kwa walengwa, kutokana na mbinu shirikishi zinazotumika kuwaandaa walengwa kutambua umuhimu na faida ya miradi.

wataalamu wa sekta mbalimbali halmashauri ya wilaya Mtwara wakiwa katika picha ya pamoja

Ameendelea kusema kuwa elimu wanayoipata hapa inawataka kuongeza weledi na ubunifu mkubwa kwa kuwa miradi yote itakayoibuliwa na kutekelezwa na walengwa inatakiwa kufikishwa kwao kupitia elimu ya uhamasishaji ili kupata washiriki wenye morali na kazi.

hayo ya siku sita tarehe 22-27 Februari, 2021 yanafanyika katika ukumbi wa Chuo cha Walimu Kawaida Mtwara yakiendeshwa na wawezeshaji kutoka ngazi ya taifa na kufunguliwa na Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya mtwara Mikindani Bwana Orcado.

Credit: Afisa habari – Isaac Bilali