Jamii FM

KIWOHEDE yatoa Taulo za kike siku ya wanawake Duniani

6 March 2021, 14:54 pm

Siku ya wanawake Duniani imeadhimishwa leo Machi 6, 2021 katika Kata ya Nanguruwe Halmashauri ya wilaya ya Mtwara kwa taasisi na Mashirika ya mbalimbali kuwashika mkono wanawake katika kuadhimisha sikukuu hii muhimu.

Mkuu wa wilaya ya Mtwara Dunstan Kyobya akizungumza na wananchi wa Nanguruwe – Mtwara katika maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani

Mkuu wa wilaya ya Mtwara Danstan Kyobya amesema wanawake ni jeshi kubwa ambalo linapaswa kulindwa na kuhakikisha wanapata Elimu Ili wawe viongozi imara, Ametoa mfano wa viongozi mbalimbali ambao ni wanawake namna wanavyofanya Kazi na namna ambayo wamekuwa mfano wa kuigwa katika Jamii.

Miongoni mwa walioshiriki ni pamoja Devotha Raymond ambaye ni Mratibu KIWOHEDE kupitia Mradi wa Sauti mpya, wameshiriki kwa kutoa Taulo za Kike zenye thamani ya shilingi milioni Moja Kwa wanafunzi wa shule ya Msingi na sekondari Nanguruwe.

Devotha Raymond wa KIWOHEDE akikabidhi Moja ya Box zenye Taulo za kike kwa mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Nanguruwe mbele ya Mkuu wa wilaya ya Mtwara

Lengo likiwa ni kuwathamini wanafunzi wa kike katika Elimu, Ili wasiache kuhudhuria masomo kwa kisingizio cha kukosa Taulo na kushindwa kuwa huru wakati wa masomoHata hivyo Mkuu wa shule ya sekondari Nanguruwe amewashukuru KIWOHEDE na We World kwa msaada huo na kuahidi kufikisha kwa walengwa.

Mashirika mengine yaliyoathiriki katika siku hii ni pamoja na Door of hope, MDC, MSOAPO, na CWT

Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani hufanyika kila mwaka ifikapo Machi 8, ambapo Kimkoa yataadhimishwa katika wilaya ya Masasi yakiwa na kauli mbiu “WANAWAKE KATIKA UONGOZI CHACHU KUFIKIA DUNIA YENYE USAWA”