Jamii FM

Waandishi someni sheria

20 April 2021, 15:59 pm

Na Karim Faida

Waandishi wa habari Tanzania wameaswa kuzisoma na kuzielewa Sheria mbalimbali zinazohusiana na tasnia yao hasa sheria ya haki ya kupata taarifa iliyopitishwa na bunge Septemba 7 2016 na kuidhinishwa na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania hayati Dkt John Pombe Magufuli.

Katibu mtendaji wa Baraza la habari Tanzania Ndugu Kajubi Mukajanga akizungumza na waandishi

Hayo yamesemwa na Katibu mtendaji wa baraza la habari Tanzania Ndugu Kajubi Mukajanga katika mkutano wa waandishi wa habari kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania uliofanyika leo April 20 2021 katika ukumbi wa Shamool hotel jijini Dar es salaam.

Afisa program kutoka baraza la Habari Tanzania Bi Saumu Mwalimu akiwaelekeza waandishi wa Habari

Kwa upande wake Bi Saumu Mwalimu ambaye ni Afisa program kutoka baraza la Habari Tanzania, ameongeza kuwa ukizisoma na kuzijua sheria itakusaidia kufanya kazi kwa weledi na kujiamini kwa kuwa taratibu nyingi unazifahamu.

Katibu mkuu wa Jukwaa la wahariri Tanzania Ndugu Nevil Meena

Hata hivyo Katibu mkuu wa Jukwaa la wahariri Tanzania Ndugu Nevil Meena katika kuiangalia sheria hiyo ya haki ya kupata taarifa amesema baraza la habari Tanzania MCT wamefanya utafiti kwa waandishi 73 kutoka vyombo vya habari 56 kutoka mikoa 6 ya Tanzania kujua kwa namna gani waandishi wana uwelewa kuhusu sheria hiyo na 67% ya waandishi wanafaham kuwepo kwa sheria hiyo.

Waandishi wa Habari walifuatilia maelezo yanayotolewa

Jumla ya waandishi wa 33 kutoka mikoa mbalimbali wameshiriki kutoka vyombo tofauti kama vile waandishi wa Magazeti, Radio, Televisheni, katuni na wale wa Online.