TOVUTI YA REDIO MUBASHARA
Kahama FM

TADIO yazitaka Redio za kijamii kuchangamkia nguvu ya Teknolojia.

March 24, 2021, 10:51 am

Radio za kijamii nchini zimetakiwa kutumia tovuti ya kurusha matangazo mubashara ya TADIO kuibua na kutatua changamoto mbalimbali zilizopo katika jamii zao ikiwa ni Pamoja na kutanua wigo wa masoko katika kukuza kipato cha radio hizo.

MKUFUNZI WA NDANI KUTOKA TADIO AMUA RUSHITA AKITOA SOMO LA TOVUTI YA REDIO MUBASHARA.

Wito huo umetolewa leo jijini mwanza na Mkufunzi wa ndani wa mafunzo ya siku mbili ya matumizi ya tovuti ya kurusha matangazo mubashara ya TADIO  Amua Rushita yaliyoshirikisha redio jamii kutoka Mkoa wa Shinyanga,Geita,Simiyu na Mara.

Rushita amesema kuwa matumizi ya Kikapu cha redio inasaidia Habari kufika mbali hali inayosaidia watoa maamuzi kuziona changamoto zilizopo katika jamii na kuzitolea ufumbuzi.

Katika hatua nyingine amewataka wamiliki wa redio za kijamii kutumia tovuti ya kurusha matangazo mubashara ya TADIO kutafuta masoko kwakuwa mtandao huo unawafikia watu wengi wanaohitaji kutangaza na redio za kijamii.

Kwa upande wao baaadhi ya waandishi wa Habari walioshiriki mafunzo hayo wameishukuru TADIO kwa kuwapa elimu hiyo na kusema kuwa itawasaidia pia kuongeza wigo wa kufahamika katika maeneo mbali mbali ambako hawajulikani.

Akifafanua redio shiriki za mafunzo hayo,Afisa Tehama wa Mtandao wa Redio za kijamii Kutoka TADIO Ayubu Lulesu amesema kuwa Mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na Shirika la VIKES kutoka Finland limeshirikisha Redio kumi ambazo ni Kahama Fm,Sengerema Fm,Mazingira Fm,Sibuka Fm na Storm Fm.

Zingine ni Huheso Fm,Karagwe Fm,Kwizera Fm,Uvinza Fm Pamoja na Uyuwi Fm.