Kahama FM

Kikosi cha 23 KJ Kimehitimisha mafunzo rasmi ya Sambalatisha Adui.

April 29, 2021, 10:08 am

Jeshi la wananchi wa Tanzania  kikosi cha 23 KJ  limehitimisha mafunzo rasmi ya sambalatisha adui  yaliyolenga kujikumbusha mbinu mbalimbali za kivita  ikiwa ni pamoja na kujiweka timamu kila wakati  ili kuendelea kulinda mipaka ya nchi .

Picha ya wanajeshi wakiwa katika mazoezi (Picha hii haihusiani na habari hii)

Mkuu wa shule ya ifantiria Brigedia Jenerali  Selemani Gwaya ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mazoezi   hayo ,amewataka  askari  walioshiriki  mafunzo hayo kuendelea kufanya mazoezi zaidi kwa kuzidisha muda wa kuwepo kambini ili kujiweka timamu na kuhakikisha mipaka ya nchi inakuwa salama

Sauti ya Brigedia Jenerali Selemani Gwaya.

Kwa upande  wake  kamanda wa vikosi vya magharibi  Brigedia Jenerali  Julius Gambusi  amesema  mafunzo hayo wamepata uzoefu ,katika maeneo ya mbinu za kivita ,uvumilivu ,utimamu wa mwili  na usimamizi  wa vikundi katika ngazi mbalimbali.

Sauti ya Kamanda wa vikosi vya magharibi  Brigedia Jenerali  Julius Gambusi 

Nao baadhi ya askari  walioshiriki  mafunzo ya sambalatisha adui kwa mwaka 2021  Luteni  Ussu  Melania Rwekiiza ,Luteni ussu  Happyness  Paulo Luteni ussu Fatuma  Othman wamesema  wamefurahishwa na mazoezi hayo ambayo yamefanyika kwa vitendo huku wakiahidi kuendelea kujinoa zaidi

Sauti za askari walioshiriki mafunzo hayo