soko la sango
Kahama FM

Wafanyabiashara wa Soko la Sango Kahama waiomba serikali Kuboresha Miundombinu.

May 26, 2021, 7:42 am

Wafanyabiashara katika eneo la PHATOMU wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameiomba serikali kuboresha miundombinu katika soko la SANGO lililopo kata ya NYASUBI manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga, baada ya kuondolewa katika eneo hilo, na Mtendaji wa kata, na kutakiwa kwenda katika maeneo mengine walilopangiwa na serikali.

Wafanyabiashara wa Soko la Sango Kahama.

Wakizungumza leo na KAHAMA FM wafanyabiashara hao wamesema Miundombinu ya Soko hilo bado ni mibovu, ambapo soko hilo linaukosefu wa maji safi na salama, choo, pamoja na ulinzi wa vifaa vyao.

Sauti ya wafanyabisahara wa soko la Sango.

Kwa upande wao wafanyabiashara katika soko la SANGO wamekiri kuwepo kwa miundombinu mibovu Sokoni hapo, huku wakimlalamikia mzabuni kufunga choo kwa madai kuwa mauzo hayamlipi, ambapo imewalazimu kujisaidia katika vyumba vyilivyokuwa wazi.

Wafanyabiashara wa soko la Sango.

Mtendaji wa kata ya nyasubi INNOCENT KAPERE amesema wamepangiwa maeneo ya kufanyia biashara ikiwemo soko la CDT, MAJENGO, soko la SANGO na masoko mengine yaliyopo katika manispaa ya Kahama, ambapo pia amewataka kutekeleza maelekezo yaliyotolewa na serikali.

Sauti ya Mtendaji wa Kata Innccent Kapere

Aidha INNOCENT amesema choo kilichopo sango kimefungwa kutokana na kukusekana kwa watumiaji.

Sauti ya Mtendaji wa Kata Innccent Kapere

Hata hivyo,SOKO la sango lililopo kata ya Nyasubi manispaa ya kahama, halijafanyiwa ukarabati kwa muda mrefu.