Kahama FM

Halmashauri ya Manispaa ya Kahama yapongezwa kwa kuelekeza fedha za mapato ya ndani kwenye miradi ya maendeleo

June 1, 2021, 6:04 pm

Halmashauri ya manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga imetakiwa kuendelea kutekeleza miradi mbalimbli ya maendelea kwa kutumia mapato ya ndani ili kutatua changamoto za wananchi.

Kauli hiyo imetolewa leo na waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) UMMY MWALIMU, wakati akikagua miradi mbalimbali ya maendeleo, ambapo amepongeza manispaa ya Kahama kwa kuelekeza fedha za mapato ya ndani kwa kufanya miradi ya maendeleo.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kahama ANNAMRINGI MACHA amesema kuwa lengo la kujengwa kwa kituo cha afya Nyasubi ni kupunguza mlindukano wa wangonjwa hasa wakina mama na watoto katika Hospitali ya wilaya ya Kahama.

Naye mganga mkuu wa halmashauri ya manispaa ya Kahama Dr DAVID LUCAS amesema kuwa tangu waanze kutoa huduma ya nje katika kituo hicho cha afya wameweza kuhudumia wagonjwa wapatao 400 hadi 500.

I

Kwa upande wake diwani wa kata ya Nyasubi ABELI SHIJA amemuomba waziri UMMY MWALIMU kujengewa uzio kwa ajili ya ulinzi wa wagonjwa pamoja na kupata sehemu ya kujenga nyumba ya dakari katika kituo hicho.