Kahama FM

Madiwani, watendaji na wawezeshaji katika halmashauri ya ushetu watakiwa kutoa ruzuku kwa kuzingatia sifa.

July 7, 2021, 4:27 pm

Madiwani, watendaji na wawezeshaji katika halmashauri ya ushetu wilayani kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kutoa ruzuku kwa kaya masikini kupitia TASAF kwa kuzingatia sifa za watu wanaopaswa kupata ruzuku hiyo, kwa uadilifu na kuzingatia taratibu, kanuni na sheria za utoaji fedha hizo.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa tarafa ya Dakama TUMSHUKURU MDUI akimwakilisha mkuu wa wilaya ya Kahama, katika ufunguzi wa kikao kazi cha kuwajengea uelewa kwa sehemu ya pili ya awamu tatu ya TASAF, kwa madiwani, watendaji na wawezeshaji ambapo amesema wanapaswa kufanya kazi kwa uadilifu.

Kwa upande wake Afisa kutoka makoa mkuu ya TASAF kitengo kinachoshughulikia malipo kwa njia ya kietroniki JOSEPHINE JOSEPH amesema kuwa kwa kipindi hiki TASAF itanufaisha kaya ambazo zinaoishi kwenye mazingira duni ili kuziondoa kwenye umasikini.

Naye, mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya ushetu MARCO MATOMOLA amewataka viongozi wa kisiasa kuwasaidia wananchi ambao wanaishi katika umasikini kwa kuwapatia ruzuku hiyo.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Nyamilangano ROBART MIHAYO ameshukuru TASAF kwa kuviingiza vijiji nne vya kata yake kwenye mpango huo wa sehemu ya pili ya awamu ya tatu.

INSERT………. MIHAYO

Hata hivyo, TASAF katika tathimini ya utekelezaji wa kipindi cha awamu ya tatu imeonyesha kuwa mradi huo umechangia katika kufikiwa kwa azma ya serikali ya kupunguza umasikini nchini.