KAHAMA
Kahama FM

KATAMBI:Vijana bila kuwa na Malengo na Kujitolea kwanza kutoboa ni ngumu.

July 15, 2021, 2:02 pm

Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi

KAHAMA:

Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi amewataka Vijana wa Tanzania kuwa na malengo katika Maisha yao ikiwa Ni pamoja na kuanza kufanya kazi kwa kujitolea katika mashirikia na ofisi Mbalimbali.

Katambi ameyasema hayo Leo wakati akizungumza kwa njia ya simu na Kipindi Cha Ukurasa Mpya Cha Kahama Fm wakati dunia inaadhimisha siku ya Ujuzi wa Vijana Duniani.

Katambi Amesema kuwa vijana wengi wanakuwa na Maisha magumu kutokana na Kushindwa kuwa na malengo pamoja na kuwa na ndoto za kuwa na Maisha mazuri pasipo kufanya  kazi.

Sambamba na hayo Katambi amewataka vijana kujiunga kwenye vikundi na kufuatilia mikopo ya asilimia 5% inayotolewa na halmashauri kwa vijana.

Kuhusu Matumizi ya dawa ya kulevya Katambi amewaasa vijana kuacha kutumia kwani hayana faida yoyote na kwamba Serikali kwa Sasa inakabiliana na madawa ya kulevya kwa kuwakamata wauzaji,wasambazi na watumiaji wa dawa za kulevya.

Siku ya Ujuzi wa Vijana huazimishwa kila ifikapo July 15 ikiwa Ni kutambua mchango wa Ujuzi wa Vijana katika nyanja Mbalimbali za kuleta Maendeleo.