chuo
Kahama FM

Wahitimu vyuo vikuu walazimika kuolewa kutokana na kukosa ajira mtaani.

July 15, 2021, 8:41 am

Wanawake waliohitimu vyuo  vikuu nchini wamesema wanalazimika kuingia kwenye ndoa ili kujikwamua na ugumu wa maisha wanapofika mtaani baada ya kukosekana kwa ajira licha ya kuwa na elimu ya juu.

Hayo yamebainishwa na baadhi ya wadau mjini Njombe wakati wakitoa maoni yao juu ya mwenendo wa elimu ya Tanzania huku wakitoa wito kwa wanafunzi waliochaguliwa kwenda kujiunga na vyuo vikuu kuchagua fani zitakazoweza kuwapa nafasi za kujiajiri mtaani pindi wanapokosa ajira.

Tofana Pascali ni mmoja wa wanawake wasomi aaliyesoma maendeleo ya jamii anasema wanawake wasomi baada ya kumaliza vyuo vikuu wanalazimika kuishi na wanaume watafutaje watakaowawezesha kupata chochote katika maisha yao.

“Mwanaume atahangaika ataleta chochote kile nyumbani tule tulale ili maisha yaende kwasabau hata wazazi mtaani wamechoka kuombwa ndio maana tumeona ni bora tujiegeshe kwa wanaume hata kama hawajaonekana na mwisho wa siku wanatokea hata watoto wa mtaani”alisema Tofana

Emmanuel Ngelime na Johnson Mgimba ni miongoni mwa wadau wa elimu wanatoa wito kwa wanafunzi kuwa na machaguo sahihi wanapokwenda vyuoni ili wafanikiwe kuwa na shughuli za kufanya mtaani.

“Wasomi wengi sana wako mtaani kwa kukosa ajira,ninaomba wanafunzi wawe makini na hizi taaluma wanazozichagua lakini pia serikali iongeze nguvu kwenye vyuo vya maendeleo na VETA ili tuweze kupata wataalamu zaidi”alisema Ngelime

Naye Mgimba amesema “Tunaiomba serikali kwasababu ya changamoto hii ya ajira basi yale masomo ambayo tunajua motto akimaliza anweza kujiajiri basi wajaribu kuyapa kipaumbele kwenye swala la mkopo ili watoto wahamasike waweze kwenda kwenye yale masomo ili akimaliza na akakosa ajira basi aweze kujiajiri”alisema Mgimba

Alatanga nyagawa ni mhadhiri wa chuo cha Amani mjini Njombe ameiomba serikali kubadili mtaala wa elimu ili wanafunzi waweze kusoma masomo yatakayoendana na mazingira ya Tanzania na kujiajiri.

“Tunakwenda na masomo ambayo yanahitaji ukimaliza utembee na bahasha uombe ajira kwenye ofisi ya mtu,nadhani tuna changamoto kubwa kwenye silabasi zetu .Jambo hili tunahitaji kuliangalia upya ili tuhame na kwenda kwenye uhalisia wa maisha yetu”alisema Alatanga Nyagawa

Credit:Muungwana Blog