kahama
Kahama FM

KAHAMA:Wafanyabiashara wakoshwa na serikali ya awamu ya Sita,Wasema kazi iendelee.

July 19, 2021, 2:35 pm

Mkurugenzi wa Kampuni ya Kahama Huduma,Bwana Charlse Daudi.

KAHAMA:

Wafanyabiashara MANISPAA ya Kahama Mkoani Shinyanga wameipongeza Serikali ya awamu ya Sita chini ya RAIS Samia Suluhu Hassan kwa kuwapa nguvu ya kufanya biashara zao kwa uhuru na kufuata taratibu za Serikali.

Hayo yamebainishwa leo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Kahama Huduma  Charles Daud alipokuwa ikitoa neno la shukrani kwa niaba ya wafanyabiashara  Katika Kikao Cha maandalizi ya maonesho ya uwekezaji na Biashara Kahama.

Daudi Amesema kuwa kwasasa wafanyabiashara wanafanya kazi kwa amani na kwamba wanapata ushirikiano Mkubwa kutoka kwa tasisi za Serikali na wamemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mh Kiswaga kwa kuwatia moyo.

Sauti ya Mkurugenzi wa Kahama Huduma,Bwana Charles Daudi.

Katika hatua nyingine Wamekishukuru Kituo Cha uwezeshaji kiuchumi na uongozi wa Manispaa ya Kahama kwa kuleta maonyesho hayo na kwamba itawasaidia Kupata mbinu mpya na kutanua masoko.

Picha ya Pamoja Mara baada ya kikao cha Maandalizi.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kahama Festo Kiswaga amesema kuwa kwa mara ya kwanza mwaka huu katika maonesho hayo yataambatana na shindano la walipa kodi wakubwa na amewaagiza mamlaka ya mapato Tanzania TRA mkoa wa kikodi Kahama kuanza kuandaa zoezi hilo.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya Ya Kahama Festo Kiswaga.

Sambamba hayo Kiswaga amesema kuwa hataki kusikia Biashara yoyote imefumgwa Kahama na kwamba kufungwa kwa biashara kunasababisha kurudisha nyuma  uchumi wa mtu mmoja moja na na nchi.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya Ya Kahama Festo Kiswaga.

Maonesho ya uwekezaji na bishara Kahama yataanza Tarehe 30 mwezi wa 7 Hadi Tarehe 8 mwezi wa 8 na yatakuwa yakifanyika usiku na Mchana yakiwa na kauli mbiu isemayo Kahama,Kitovu cha biashara ukanda wa maziwa makuu.

Baadhi ya wajumbe wa kikao cha maandalizi wakimsikiliza kwa makini mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga,Hayupo Pichani.