Mazingira FM

Billioni 1 kujenga makao makuu ya halmashauri.

2 April 2021, 5:27 pm

  1. Halmashauri ya wilaya ya Bunda mkoani Mara imepokea kiasi cha pesa za KitanzaniaTsh. Billioni Moja kwa ajili ya ujenzi wa makao makuu ya halmashauri hiyo.
Kaimu mkurugenzi Halmashauri Wilayaya Bunda Staffa Nashon

Taarifa ya kupokea pesa hizo imetolewa katika kikao cha baraza la madiwani kwenye kikao cha robo ya pili ya Mwaka na kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Staffa Nashon

Hata hivyo Nashon amewaomba waheshimiwa madiwani kuacha malumbano ya wapi halmashauri hiyo ijengwe na badala yake wajielekeze kwenye ujenzi ili waweze kukamilisha ujenzi huo kwa wakati.

Halmashauri ya wilaya ya Bunda ilipokea Barua kutoka ofisi ya katibu mkuu TAMISEMI ikielekeza kujengwa makao makuu ya halmashauri hiyo eneo la Kibara stoo kata ya Kibara Tarafa ya Nansimo.