Mazingira FM

Waliokimbia ukeketaji Mara waendelea na maisha

14 April 2021, 8:09 am

Katika mila za kikurya, kizanaki na kiikizu  mkoani Mara moja ya Mila yao kubwa ilikuwa ni ukeketaji huku sababu kuu ikielezwa kuwa ni kutengeneza nidhamu miongoni mwa wanawake huku bila kutathmini madhara yanayoweza kujitokeza kwa wanawake pindi wanapofanyiwa kitendo hicho cha kikatili

baadhi ya vifaa vinavyotumika kukeketa

Anna mnyika mkazi wa maliwanda halmashauri ya Mji wa Bunda ambapo kabila lake ni mzanaki kabila ambalo ni miongoni mwa yale yanayotekeleza mila za ukeketaji katika mkoa wa Mara anaeleza jinsi gani alivyonusurika kukeketwa hasa baada ya kushuhudia mwenzake akitokwa na damu nyingi baada ya kufanyiwa kitendo hicho 

Catherine Kilemba pia ni mkazi wa Maliwanda Halmashauri ya Wilaya ya Bunda ambaye kabila lake ni Mwikizu anaeleza pia kwa upande wake alivyoyakimbia madhira haya ya ukeketaji katika jamii yake na kuamua kwenda kuishi mjini kwa kipindi kilefu zaidi akiogopa kukeketwa

Mbali na masuala ya ukeketaji kutajwa kama sehemu ya jamii hizi za watu wa Mara kuchukua nafasi kubwa lakini pia wengi wanataja kuwa ilikuwa ni shinikizo kwa familia ili binti aweze kuolewa mapema pia kushiriki shughuri za kijamii kama wengine. Kwa anna mnyika pamoja kwamba hakufanyiwa ukeketaji lakini ameweza kuolewa  mapema na mahali imeweza kutolewa kwa familia.