Mazingira FM

Diwani wa bunda stoo atoa mifuko 5 ya saruji ujenzi wa choo shule ya miembeni

7 June 2021, 5:53 pm

Diwani wa kata ya Bunda Stoo Flavian Chacha ametoa mifuko mitano ya saruji katika kuunga juhudi za wananchi za ujenzi wa choo cha shule ya msingi miembeni

Diwani wa Bunda stoo Flaviani Chacha akikabidhi cement kwa shule ya Miembeni

Katika ujumbe wake diwani huyo amesema ameona ni vyema kushiriki juhudi za wananchi kwenye ujenzi huo wa choo kwa kuwa hapendi kuona shule inafungwa kwa kukosa choo hivyo anawaomba wadau wengine kuendelea kujitolea kuisaidia serikali na wananchi ili kulenta maendeleo kwa jamii

shimo la choo ambacho kinajengwa kwa nguvu za wananchi shule ya msingi Miembeni Pichani ni Diwani na viongozi wa shule

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule ya msingi Miembeni A David Magesa amesema shule ya miembeni yenye A na B kuna jumla ya wanafunzi 2500 hivyo uhitaji wa vyoo kwa shule zote mbili A na B ni zaidi ya matundu 100 hivyo amemshukuru diwani kwa kujitolea kuchangia maendeleo ndani ya kata yake

Naye mwenyekiti wa ujenzi wa choo hiyo ndugu Emmanuel Nyamonge amesema ujenzi huo ulianza mwezi wa tisa mwaka jana na juhudi za wananchi zinatumika ambapo kila kicha cha mtoto huchangia kiasi cha shilingi 5500 na ujenzi huo umepagwa kugharimu shilingi milioni 12 ambapo mpaka sasa imepatikana shilingi million 4 tu