Nuru FM

Watoto wa mitaani waiomba serikali iwapatie bima za afya

16 April 2021, 7:35 am

Watoto wanaoishi na kufanya kazi mtaani Manispaa ya Iringa wameiomba serikali kuwakatia bima za afya zitakazo wawezesha kupata huduma pindi wanapokutana na changamoto za kiafya.

Wakizungumza na nuru fm baadhi ya watoto hao wamesema kuwa ni vyema serikali ikawakatia bima zafya ili wapate huduma kwa uharaka kutokana na ugumu wa maisha huku wakiiomba jamii inayowazunguka kuwajali na kuwaamini

Sauti Watoto

Kwa upande wake Mama nyagawa ambaye ni afisa maendeleo amesema kuwa watoto wanaoishi na kufanya kazi mtani hawapaswi kukata tama pamoja na kuiasa jamii kuachana na majina mabaya waliyokuwa wakiwaita kwani ni udharirishaji

Afisa maendeleo

Kwa upande wake Afisa afya manispaa ya iringa David Mpagama amesema kuwa serikali itahakikisha inawapatia Bima za afya watoto hao ili kulinda afya zao pindi wanapougua.

Extended fabiola