Radio Fadhila

WADAU wa elimu Jimbo la Lulindi Halmashauri kupiga marufuku vitendo kuwafanyia sherehe watoto wao kumaliza elimu ya msingi

17 February 2021, 9:52 AM

WADAU wa elimu Jimbo la Lulindi Halmashauri ya wilaya ya Masasi mkoani Mtwara kwa kauli moja wamepitisha maazimio mbalimbali likiwemo la kupiga marufuku vitendo vinavyofanywa na baadhi ya wazazi wa wanafunzi wa wanaomaliza elimu ya msingi( Darasa la saba) kuwafanyia sherehe watoto wao kumaliza elimu hiyo. Wadu hao wamesema wapo wazazi ambao siku ya mitihani ya kuhitimu watoto wao wa darasa la saba wamekuwa na utamaduni wa kuwafanyia sherehe mbalimbali za kumaliza elimu ya msingi huku baadhi ya wazazi hao wamekuwa wakikusanyika nje ya shule kuwasubiri watoto wao wanaokuwa bado wapo katika vyumba vya mitihani wakiendelea kufanya mitihani ili wakitoka basi wa wabebe kwenye vyombo vya moto na kuwashangilia , jambo hilo limetajwa kuwa limekuwa likiwaathiri watoto kisaikolojia na kusababisha watoto kutofanya vizuri mitihani yao. Marufuku hiyo imetolewa jana katika kikao cha uboreshaji wa elimu kilichofanyika katika Jimbo la Lulindi ukumbi wa miduleni wa Halmashauri hiyo, kikao ambacho kiliwakutanisha wadau mbalimbali wa elimu , wakuu wa shule za Sekondari,Msingi, Madiwani kutoka jimbo hilo, waratibu kata elimu, watendaji wa vijiji, viongozi wa dini, wakuu wa idara wa Halmashauri hiyo pamoja na mafisa elimu Msingi na sekondari, mgeni rasmi wa kikao hicho ni mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Ibrahimu Chiputula ambaye pia ni diwani kata ya Mpeta. Wadau hao wamependekeza kuwa wazazi ambao watakaidi marufuku hiyo wachukuliwe hatua kali za kisheria ,aidha katika majadiliano ya kikao muhimu zimetajwa baadhi ya sababu ambazo zinachangia kushuka kwa hali ya taaluma kwa Halmashauri ya wilaya ya Masasi. Moja ya sababu kubwa ambayo imetajwa na wadau hao ni baadhi ya wazazi kuwashawishi watoto wao kutofaulu mitihani yao ya kitaifa yaani ule wa darasa la saba pamoja na kidato cha nne. Akichangia hoja katika kikao hicho, Diwani wa kata ya Lupaso ,Douglas Mkapa amesema kunabidi kuwepo kwa sheria ndogo ambayo wazazi kama hao wakibainika basi wafungwe jela kuanzia miezi mitatu hadi sita ili kukomesha tabia hiyo ambayo imeota mizizi kwa wazazi hatimaye kuwa fundisho kwa wengine. Hoja zingene zilizojadiliwa ni tatizo la mimba kwa wanafunzi, utoro na mahusiano ya ufanyaji kazi baina ya walimu kwa walimu. Halmashauri ya wilaya ya Masasi imeamua kufanya kikao cha uboreshaji wa elimu jimbo kwa jimbo na imeanza jimbo la Lulindi na siku chache baadae utafuatiwa na jimbo la Ndanda lengo ni kuboresha wa hali ya elimu kwa kupandisha ufaulu zaidi, katika mwaka 2020/2021 Halmashauri haijafanya vizuri katika mitihani ya kitaifa , Darasa la saba,kidato cha nne,cha pili ……..

13Daud Mnonjela, Frank S. Ndanganile na Wengine 11Maoni 6Imeshirikiwa mara 1PendaMaoniShiriki