Radio Fadhila

CHAMA kikuu Cha Ushirika wa wakulima Mtwara-Masasi ( MAMCU) kimezindua rasmi ujenzi wa ghala

20 April 2021, 5:10 AM

CHAMA kikuu Cha Ushirika wa wakulima Mtwara-Masasi ( MAMCU) kimezindua rasmi ujenzi wa ghala kubwa la kisasa la kuhifadhia mazao mbalimbali yaliyo katika mfumo wa stakabadhi mazao ghalani ikiwemo korosho lenye uwezo wa kuhifadhi mazao tani zaidi ya 5000

Ujenzi wa ghala hilo utagharimu zaidi ya Sh.750 milioni hadi kukamilika kwake, ghala hilo limejengwa katika kijiji cha Ndwika, kata ya Mangaka wilayani Nanyumbu mkoani Mtwara.

Lengo kuu la ujenzi wa ghala hilo wilayani Nanyumbu ni kuongeza uzalishaji wa mazao kwa wakulima, kupunguza umbali wa usafirashaji wa mazao ambapo awali mazao ya wakulima wa Nanyumbu walilazimika kupeleka hadi wilayani Masasi.

Ujenzi huo hadi sasa umeshafikia asilimia 87 ya kukamilika kwake. Aidha, faida nyingine ambayo itapatikana kupitia mradi huo wa ujenzi wa ghala ni fursa za kiuchumi kwa wananchi waishio karibu na ghala hilo. Hafla fupi ya uzinduzi wa ghala hilo ilifanyika jana katika kijiji cha Ndwika wilayani Nanyumbu,

mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa ni mkuu wa mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa ambapo aliambatana na watendaji wa Mamcu.

chanzo Hamisi Abdelehemani Nasiri