Sengerema FM

Waziri Aweso azinguana na watumishi 8 wa maji Mwanza

26 April 2021, 8:57 am

Waziri wa maji Jumaa aweso akikagua mradi wa maji Nyampande Sengerema uliogalimu pesa kiasi cha bil.1.8/=

Waziri wa maji Jumaa aweso ameangiza kuwekwa ndani watumishi saba wa maji mkoa wa Mwanza kufatia kuwepo na utekelezaji mbovu wa miradi ya maji wilayani Sengerema.

Waziri aweso amefikia uamzi huo baada ya kukuta miradi mingi ya maji haijakairika wilayani hapo huku mingine ikitekelezwa kinyume na BOQ  ambapo miongoni mwa miradi hiyo ni mradi wa maji Nyampande uliongarimi fedha Zaidi ya shilingi billion 1 bila kuanza kutoa maji hali inayo walizimu wananchi kuchota maji ya kunywa kwenye madimbwi.

Awali akitoa taarifa ya baadhi ya miradi iliyoleta changamoto kwa wananchi, Mbunge wa jimbo la Sengerema Mh. Hamis Tabasam Pamoja na diwani wa kata ya Tabaruka mjini Sengerema Mh. Sosipiter Simon Busumabhu wamesema kuna miradi mingi wilayani hapo iliyotekelezwa chini ya kiwango na mingine haijakamilika kwa mda mrefu sasa.

Kufatia kuwepo kwa hali hiyo Waziri  Aweso akamtaka mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela kuwaweka Ndani Mkurugenzi wa mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Mwanza(Mwauwasa),Leonard Msenyele, meneja wa wakala wa maji vijijini mkoa wa Mwanza Eng.Immaculata Raphael na meneja wa maji vijijini Sengerema (Ruasa) Eng. Cassian Augostine Wittike Pamoja na meneja wa maji mjini Sengerema Eng. Robert Lupoja, sambamba na kuvunja bodi ya maji Wilayani hapo.