Sibuka FM

WANAFUNZI SIMIYU WAOMBA KAMBI ZA KITAALUMA ZIWE ENDELEVU

16 April 2021, 11:09 am

Wanafunzi wa shule ya sekondari Bariadi mkoani Simiyu wameomba viongozi wa mkoa na wadau wote wa elimu kuwa kambi za kitaaluma ziwe endelevu kwa kuwa zina matokeo chanya kwa katika ufaulu wa wanafunzi na ili mkoa uendelee kufanya vizuri katika mitihani yote ya Kitaifa.

Ombi hilo limetolewa mapema leo hii wakati wanafunzi hao wakipokea msaada wa chakula, shajala na taulo za kike kutoka Benki ya TPB vyote vikiwa na thamani ya shilingi 4,550,000/= ambavyo vimetolewa kwa jili ya wanafunzi wa kambi za kitaaluma kwa kidato cha sita mkoani hapa.

Wanafunzi hao wamesema kuwa wanashukuru kwa msaada wa vitu walivyopewa lakini pia wanashukuru kwa jitihada za mkoa kuanzisha kambi ambazo zimesaidia kuongeza ufaulu, pamoja na ufaulu kambi hizo pia zimesaidia wanafunzi wengi kumaliza masomo yao pasipo kukatishwa na sababu za kijamii kwani muda mwingi wanakuwa shuleni,

May be an image of 10 people, people standing and outdoors
Wanafunzi wa Bariadi Sec wakipokea msaada
May be an image of 18 people, child, people sitting, people standing and outdoors
Wanafunzi wa Bariadi Sec wakiwa wanasikiliza