Sibuka FM

Zaidi ya Ng’ombe laki tatu kuchanjwa wilayani Maswa

20 April 2021, 10:28 am

Zaidi  ya   Ng’ombe  laki   tatu  wilayani  Maswa  mkoani  Simiyu   zinatarajiwa  kuchanjwa   ili  kudhibiti  Magonjwa  ya   Mifugo  ikiwemo  Ugonjwa  wa  Mapele  ya   ngozi  ili   kuboresha  bidhaa ya  ngozi  na  Ushindani  wa  Soko..

Akitoa  taarifa  kwa  Mkuu  wa  wilaya  ya  Maswa   Mh  Aswege  Kaminyoge,  Daktari  wa  Mifugo   wa  wilaya   Dokta  James   Kawamala  amesema kuwa   endapo  wafugaji  watashindwa  kuchanja   wataendelea  kuhatarisha   Maisha  ya   wanyama  hao.

Sauti ya Dokta wa Mifugo James Kawamala

 Sister  Rozamisti  Kasambu  ni  Daktari  wa  Mifugo na  Afisa  Mfawidhi  Kanda  ya  Ziwa  amesema  kuwa  mfugaji  yoyote  ni  lazima  awapende  mifugo  wake  kwa  kuwapeleka  kwenye  Chanjo  zinazotolewa  na  wataalamu  wa  mifugo.

Sauti ya Sista Rozamisti Kasambu.

 Akizindua  zoezi   hilo  la  chanjo  ya  Mifugo  Mkuu  wa   Wilaya  ya  Maswa  Mh  Aswege  Kminyoge  amesema  kuwa  kila  mfugaji  ahakikishe  anapeleka  Mifugo  yake  yote  kwenda  kuchanjwa  bila  kuacha baadhi  ya   mifugo  Nyumbani ..

Sauti ya DC Maswa Aswege Kaminyoge
DC- Maswa

Mwenyekiti  wa  Halmashauri  ya  Wilaya Paul  Simon Maige   na Mwenyekiti  wa  chama  cha  Mapinduzi   Paul   Jidayi   wamesema  kuwa Zoezi  ni  la  Muhimu hivyo ni  vyema  kufuata  maelekezo  ya  Wataalamu.

Sauti ya Mw/kiti wa Halmashauri na Mw/kiti wa Ccm-Maswa

Aidha  kwa  upande  wa   wafugaji  wameishukuru  Serikali  kwa  kusimamia  zoezi  hilo  la  Chanjo  kwani  litasaidia  Kuboresha  mifugo  yao..

Sauti ya Wafugaji -Maswa

Mtaalamu wa Mifugo
Mifugo