Sibuka FM

MARA:UTALII WA NDANI WAONGEZA LICHA YA COVID-19

27 April 2021, 8:47 pm

Idadi ya watalii wa ndani kutembelea na kujionea vivutio mbalimbali imeendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka katiaka hifadhi ya taifa ya Serengeti iliyopo mkoani Mara licha uwepo wa changamoto wa janga la Covid-19 ambapo nchi mbalimbali ulimwengu zinakabiliana na janga hili.

Hayo yamesemwa na afisa uhifadhi kitengo cha utalii katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti James Nahonyo wakati akizungumza na waandishi wa Habari wa mkoa wa Simiyu walipofanya ziara ya kutembelea hifadhi hiyo kwa lengo la kujionea na kujifunza vivutio mbalimbali na kuongeza kuwa idadi ya watalii wa ndani imeendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka lakini kuna kila haja ya kuendelea kutoa elimu ya utalii kwa Watanzania ili wapende kutembelea vivutio vilivyopo hapa nchini hususani Serengeti kuja kujionea maajabu ya hifadhi hiyo kama msafara wa mnyama Nyumbu.

Insert ya James Nahonyo 1

Nahonyo ameongeza kuwa pamoja na mafanikio makubwa ya kuongezeka kwa idadi ya watalii wa ndani katika hifadhi hiyo lakini amekiri kuathirika kwa utalii hasa kwa watalii kutoka nje ya nchi hasa kipindi hichi ambapo dunia nzima inakabiliana na janga la Covid-19 ambapo idadi ya watalii  kutoka nje ya nchi imepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na baadhi ya nchi kufunga mipaka yake.

Insert ya James Nahonyo 2

Kwa upande wake afisa uhifadhi idara ya Ikolojia Seph Flowin Choma amesema kuwa kazi ya idara ya Ikolojia ni kuhakikisha mahitaji yote ya msingi ya Wanyama yanapatikana pamoja na mwingiriano wa viumbe hai na visivyo hai unaendelea kuwepo katika hifadhi hiyo.

Insert ya Seph Choma

Hifadhi ya taifa ya Serengeti iliyo na ukubwa wa kilomita za mraba 14,763 na ni ya tatu kiukubwa hapa nchini ukitoa hifadhi ya taifa ya Nyerere na Ruaha na ni moja ya hifadhi ambayo imeshinda tuzo mbili kwa miaka miwili mfululizo kama hifadhi bora Afrika mwaka 2019 na 2020.