Sibuka FM

TMDA UTUNZAJI WA KUMBUKUMBU BADO NI CHANGAMOTO

11 May 2021, 8:13 am

Meneja wa mamlaka ya dawa na vifaa tiba (TMDA) Sofia Mziray amesema bado kuna changamoto ya utunzaji wa kumbukumbu dawa zenye madhara ya kulevya.

Kwenye picha ni meneja wa TMDA kanda ya ziwa Sofia Mziray akisalimiana na kaimu katibu tawala mkoa wa Simiyu Ekwabi Mujungu baada ya kumalizika kwa kikao kazi cha utunzaji wa kumbukumbu za madawa na utambuzi wa dawa zenye asili ya kulevya

Ameyasema hayo  kwenye kikao kazi kilichowakutanisha watumishi wa sekta ya afya na mifugo  ambacho kimefanyika kwa muda wa siku mbili kuona namna ya kufanya shughuli za uthibiti  lengo likiwa  kuona mkoa wa Simiyu na kanda ya ziwa kwa ujumla hakuna bidhaa zisizokuwa na ubora.

Sauti ya meneja wa TMDA kanda ya ziwa Sofia Mziray

Mziray aliongeza kuwa mara nyingi wakiwa kwenye ukaguzi wamekutana na dawa ambazo hazina ubora, bandia na ambazo hazijasajiliwa  huku akiongoza kuwa tayari TMDA imeweka wakaguzi ngazi ya mkoa ambao watasaidia kuthibiti hali hiyo.

Sauti ya meneja wa TMDA kanda ya ziwa SofiaMziray

Awali akifungua mafunzo  hayo kaimu katibu tawala mkoa wa Simiyu Ekwabi Mujungu alisema kufanya kazi bila taarifa (kumbukumbu) ni tatizo kubwa ambalo linahitaji ufumbuzi wa haraka huku akiwataka kupitia kikao kazi hicho kuja na suruhisho la kudumu.

Sauti ya kaimu katibu tawala mkoa wa Simiyu Ekwabi Mujungu

Nao washiriki wa kikao hicho walisema watayafanyia kazi yale yote yaliyoazimiwa na  kuhakikisha jamii ina kingwa na madhara yanayoweza kuepukika.

“Tumefurahisha sana na mamlaka ya uthibiti wa vifaa tiba na kinga kanda ya ziwa kutupatia mafunzo haya nasi tunaahidi kuyatekeleza yale yote ambayo tumeelewana na kuazimia kwenye kikao kazi hichi ili jamii yetu ya mkoa wa Simiyu iweze kuwa salama na kuepuka madhara yatokanayo na dawa zenye asili ya kulevya”walisema washiriki